Picha kutoka Afrika zaonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya uchoraji yaliyoandaliwa na Kituo cha Anga ya Juu cha Tiangong cha China
2023-09-15 22:26:54| cri

Kituo cha anga ya juu cha Tiangong cha China kimefanya maonyesho ya kimataifa ya uchoraji kwa mara ya kwanza, ambapo picha kutoka Afrika zimeonyeshwa kwenye maonyesho hayo.

Mwezi Machi mwaka huu, mashindano ya uchoraji yenye kaulimbiu ya “Ndoto Yangu” kwa vijana vya Afrika yalifanyika, ambayo vijana zaidi ya elfu mbili kutoka Afrika walishiriki. Picha kumi kati ya picha za washiriki hao zilichaguliwa kuingia na kuonyeshwa kwenye kituo cha Tiangong cha China, na zilipelekwa na chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-16 mwishoni mwa mwezi Mei mwaka kuu.