Walimu ni muhimu katika jitihada za kuondoa ujinga wa kutojua kusoma na kuandika
2023-09-15 09:16:15| CRI

Tarehe 10 September kila mwaka, China inaadhimisha Siku ya Walimu. Katika Siku hii, walimu nchini hapa wanajumuika na kutafakari mafanikio, changamoto, na kujadili nini kifanyike ili kuendeleza kazi hii inayopewa umuhimu mkubwa nchini humo. Wakati huohuo, September 8 ni Siku ya Kimataifa ya Kufuta Ujinga wa Kusoma na Kuandika.

Masuala haya mawili ni muhimu na yanaendana kwa kiasi kikubwa, kwani bila walimu, si rahisi kufuta ujinga wa kusoma na kuandika. Hivyo basi, katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake, tutaangazia mafanikio ya sekta ya elimu na walimu nchini China, lakini pia tutaangalia jinsi ambavyo jamii zinajitahidi kupambana na ujinga wa kutojua kusoma na kuandika.