Rais wa Tanzania awaapisha majaji 24 wapya ili kuimarisha usimamizi wa haki
2023-09-15 09:42:40| CRI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Alhamisi aliwaapisha jumla ya majaji 24, ambapo kati yao 20 ni wa Mahakama Kuu na wanne ni wa Mahakama ya Rufaa na kufanya jumla ya majaji kufikia 105, katika hatua inayolenga kuimarisha usimamizi wa haki nchini humo.

Baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam, Mama Samia aliwaambia majaji hao kwamba wana kazi kubwa mbele yao ya kufuta kesi zinazoendelea katika Mahakama Kuu na Mahakama za Rufaa. Mkuu huyo wa nchi pia aliitaka idara ya mahakama kurejesha imani ya watu kwa kufanya kazi kwa bidii katika utekelezaji wa haki.

Kwa upande wake Jaji Mkuu Ibrahim Juma, alimshukuru rais kwa kuwateua na kuwaapisha majaji wapya, akisema kwa jumla, Mama Samia ameteua majaji 19 wa Mahakama ya Rufaa na majaji 63 wa Mahakama Kuu katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya utawala wake. Jaji Juma aliwataka majaji hao kujitahidi kuwa na tabia za uadilifu, akisema watakaoshindwa watachukuliwa hatua.