Misri yapenda kushirikiana na China katika teknolojia za ulinzi wa mazingira na hali ya hewa
2023-09-15 11:11:24| cri

Waziri wa Mazingira wa nchini Misri, Bi. Yasmine Fouad ameeleza matarajio ya nchi hiyo kushirikiana na China katika teknolojia za mazingira na hali ya hewa, na kwamba kuna fursa nyingi za ushirikiano kati ya Misri na China katika nyanja za mazingira na hali ya hewa.

Bi. Fouad amesema hayo alipohojiwa na Shirika la Habari la China Xinhua, kando ya mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji katika Mazingira na Hali ya Hewa uliofanyika katika Mji Mkuu Mpya wa nchi hiyo. Amesema, teknolojia za uhifadhi wa mazingira na hali ya hewa za nchini China zinafaa kwa nchi ya Misri, na fursa za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya nishati pia zinaongezeka.