Li Xi ahudhuria Mkutano wa Kilele wa G77 na China uliofanyika mjini Havana
2023-09-17 17:19:26| CRI

Mwakilishi maalum wa Rais wa China, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Li Xi amehudhuria na kuhutubia Mkutano wa Kilele wa Kundi la Nchi 77 (G77) na China uliofanyika mjini Havana, nchini Cuba.

Kwenye hotuba yake, Li amesema hivi sasa nguvu ya nchi zinazoendelea inaendelea kuongezeka, na wakati huohuo, baadhi ya nchi zilizoendelea zinavuruga maslahi na nafasi ya kujiendeleza ya nchi zinazoendelea kwa kuweka vikwazo na kutenganisha mnyororo wa ugavu. Amesema kutokana na hilo, G77 na China zinapaswa kushikilia nia ya kulinda uhuru, mshikamano, thamani ya binadamu wote, njia ya amani katika kutatua mivutano kati ya nchi, ili kulinda kwa pamoja amani na utulivu duniani.

Aidha, Li amesisitiza kuwa ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, China daima inashirikiana na nchi nyingine zinazoendelea, bila kujali mafanikio yake katika kujipatia maendeleo.