Waziri mkuu wa China ahutubia hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 20 ya China na ASEAN
2023-09-18 08:28:32| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang jana alihudhuria hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 20 ya China-ASEAN na mkutano wa kilele wa Biashara na Uwekezaji wa China na ASEAN huko Nanning.

Akihutubia katika hafla hiyo, Bw. Li amesema uhusiano kati ya China na ASEAN umekuwa mfano wa mafanikio ya ushirikiano katika eneo la Asia na Pasifiki, hatua ambayo inahitaji juhudi za pamoja za pande zote. Amesema maneno manne yaliyotolewa kwa muhtasari na rais Xi Jinping wa China, ambayo ni upendo, unyoofu, manufaa ya pande zote na ushirikishwaji, ni mwelekeo wa msingi wa diplomasia ya kigeni ya China, na ni njia ya kuishi kwa ujirani mwema na urafiki.

Ameongeza kuwa, China itahimiza ushirikiano bora kati ya ujenzi wa pamoja wa mpango wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali.