Jengo kubwa la kihistoria mjini Khartoum lateketea kwa moto
2023-09-18 10:57:30| cri

Majengo kadhaa yameteketea kwa moto katika mji mkuu wa Sudan kutokana na mapigano makali yanayoendelea kati ya jeshi la serikali na vikosi vya upinzani.

Video zilizowekwa mtandaoni Jumapili zinaonyesha mnara wa kampuni ya mafuta ya Greater Nile Petroleum likiteketea kwa moto. Msanifu wa jengo hilo Tagreed Abdin, amesema kupitia mtandao wa X (zamani Twitter) kuwa hali hiyo inatia uchungu.

Mashambulizi ya anga na mapigano ya ardhini yameendelea kutokea Khartoum na katika miji mingine ya Sudan tangu mapigano yalipozuka mwezi Aprili.

Mnara wa kampuni ya mafuta ya Greater Nile, ni jengo la ghorofa 18 na moja ya alama muhimu zinazotambulika mjini Khartoum. Bado haijafahamika ni nini kilichosababisha moto huo, lakini hadi sasa hakuna ripoti za majeruhi au vifo.