Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning ametangaza kuwa kutokana na mwaliko wa katibu wa Baraza la Usalama la Russia Nikolai Patrushev, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya nje ya Kamati hiyo Wang Yi ataitisha mazungumzo ya raundi ya 18 ya mkakati na usalama kati ya China na Russia nchini Russia kuanzia tarehe 18 hadi 21 mwezi huu.