Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu cha Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Yi huko Malta amefanya mikutano mfululizo na msaidizi wa rais wa Marekani kuhusu masuala ya usalama wa taifa, Jake Sullivan.
Pande hizo mbili zimefanya majadiliano ya kimkakati kuhusu kuboresha uhusiano kati ya China na Marekani, ambapo Bw. Wang alisisitiza kuwa suala la Taiwan ni suala lisiloweza kukiukwa kwenye uhusiano kati ya China na Marekani. Amesema Marekani lazima ifuate taarifa tatu za pamoja kati ya nchi hizo mbili na kutimiza ahadi yake ya kutounga mkono "Taiwan kujitenga na China".