Watu wanne wauawa katika mlipuko wa bomu nchini Kenya
2023-09-18 08:40:10| CRI

Watu wanne wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya basi dogo walilopanda kukanyaga bomu lililotegwa kando ya barabara katika Kaunti ya Mandera, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Ripoti iliyotolewa na Polisi imesema, tukio hilo lilitokea jumamosi wakati basi hili lililokuwa likitokea Mandera kuelekea Kaunti ya Wajir kukanyaga bomu hilo lililotegwa na wapiganaji wa kundi la al-Shabaab.

Kaunti ya Mandera ambayo iko mpakani mwa Kenya na Somalia, ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mashambulio ya kundi la al-Shabaab.