Rwanda kutumia droni kupambana na uhalifu wa mazingira
2023-09-18 10:56:52| cri

Idara ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) na Wizara ya Mazingira ya nchi hiyo wamezindua matumizi ya ndege zisizo na rubani (droni) kupambana na uhalifu wa mazingira.

Uhalifu wa mazingira ni moja ya changamoto nne kubwa za uhalifu duniani, na uhalifu huo unaongezeka kwa asilimia tano hadi saba kila mwaka. Droni zitakusanya taarifa, kufanya ukaguzi kwa ajili ya kuzuia na kusaidia uchunguzi wa uhalifu wa kimazingira.

Waziri wa Mazingira wa Rwanda Jean d'Arc Mujawamariya amesema ndege hizo zitasaidia kukabiliana na kudhibiti shughuli zinazoharibu mazingira, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa maji, na ukataji miti katika maeneo yaliyohifadhiwa.