Mali, Niger na Burkina Faso zatangaza kuunda “Jumuiya ya nchi za Sahel”
2023-09-19 14:15:28| cri

Nchi tatu zilizoko eneo la Sahel, Mali, Niger na Burkina Faso tarehe 16 zilisaini makubaliano na kutangaza kuunda “Jumuiya ya nchi za Sahel”.

Mawaziri kutoka Mali, Niger na Burkina Faso tarehe 16 walisaini katiba ya kujenga jumuiya ya ulinzi wa pamoja huko Bamako nchini Mali. Nchi hizo tatu zinaahidi kupambana na ugaidi wa aina yoyote na uhalifu wa kupangwa ndani ya jumuiya hiyo, kitendo cha kushambulia ardhi ya nchi yoyote ya jumuiya hiyo kitachukuliwa kama uvamizi dhidi ya nchi nyingine ya jumuiya hiyo, nchi nyingine za jumuiya hiyo zina wajibu wa kutoa msaada na uokoaji, ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu. Vyombo vya habari vya Niger vimesema kusainiwa kwa makubaliano hayo kunaashiria kuwa nchi hizo tatu zinapiga hatua muhimu kwenya nyanja ya usalama na ulinzi wa pamoja.