Mkutano wa kilele wa Malengo ya Maendeleo Endelvu ya Umoja wa Mataifa wafunguliwa
2023-09-19 09:06:08| cri


 

Mkutano wa kilele wa siku mbili wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa umefunguliwa jana kwenye makao makuu ya Umoja huo, na kupitisha azimio la siasa linalolenga kuharakisha utimizaji wa malengo hayo.

Azimio hilo limeahidi kutoa fedha kwa nchi zinazoendelea, na kuunga mkono mpango uliotolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kutoa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 500 kila mwaka na utaratibu wenye ufanisi kuhusu kupunguza madeni.