China yasema iko tayari kushirikiana na wanachama wa G77 kuunda enzi mpya ya maendeleo ya pamoja
2023-09-19 08:28:02| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, Mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 77 (G77) na China uliofanyika hivi karibuni mjini Havana, Cuba, umetoa mchango chanya katika kukuza nchi zinazoendelea ili kuimarisha umoja na ushirikiano na kukabiliana kwa pamoja changamoto.

Amesema China iko tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Kundi hilo ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya Dunia ya Kusini na kuunda enzi mpya ya maendeleo ya pamoja. .

Bibi Mao pia alisema kuwa, mkutano huo wa kilele ulipitisha Azimio la Havana, linalosisitiza umoja na ushirikiano, na kukuza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa wanadamu kwa msingi wa mashauriano ya kina, ujenzi wa pamoja, na kunufaishana, kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya binadamu wote yenye mustakabali wa pamoja, na kunufaisha nchi na sehemu zote duniani.