Serikali ya China yaamua kutoa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa Libya
2023-09-19 14:15:02| cri

Shirika la ushirikiano wa maendeleo wa kimataifa la China, limesema serikali ya China itatoa msaada wa dharura wa kibinadamu wenye thamani ya yuan milioni 30 (sawa na dola milioni 4.1 za kimarekani) kwa Libya, ili kuisaidia nchi hiyo kwenye kazi ya uokoaji baada ya maafa ya kimbunga na mafuriko.

Kwa mujibu wa mahitaji ya Libya, vifaa vinavyotolewa na China ni pamoja na mahema, mablenketi, mikoba ya huduma ya kwanza, vifaa vya kusafisha maji na vifaa tiba.