Msemaji wa ujumbe wa kudumu wa China katika UM asema kupiga marufuku dawa za kulevya ni msimamo thabiti wa China
2023-09-19 22:56:06| cri

Msemaji wa ujumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa jana alipojibu swali la mwandishi wa habari kuhusu msimamo wa China katika kupambana na dawa za kulevya, alisema kupiga marufuku dawa za kulevya ni msimamo thabiti wa China wa siku zote.

Amesema China inasisitiza kuweka kinga kwanza na kupunguza mahitaji ya dawa za kulevya na siku zote inadumisha msako mkali wa kuzuia matukio ya uhalifu wa dawa za kulevya, huku ikitekeleza udhibiti mkali na ni nchi ya kwanza na pekee kwa sasa duniani kusimamia na kudhibiti kila aina ya dawa ya fentanyl, na tangu ichukue hatua hiyo, hakuna taarifa kutoka nchi nyingine kuhusu kukamatwa kwa fentanyl kutoka China.

Amesema China itaendelea kuhimiza ujenzi wa mfumo wenye ufanisi wa kupambana na dawa za kulevya duniani na kutoa wito kwa nchi mbalimbali kushirikiana kwa dhati katika jambo hilo.