Watalii wanaowasili Tanzania waongezeka na kufikia rekodi ya milioni 3.8
2023-09-20 22:35:19| cri

Idadi ya watalii wanaowasili nchini Tanzania huenda ikafikia rekodi ya milioni 3.8 mwaka huu, kutokana na kiwango kizuri cha watalii wanaoingia.

Ongezeko hili linatarajiwa kufanikisha lengo la serikali la kuvutia watalii milioni tano, ambao wataweza kuingiza pato la dola bilioni 6 za kimarekani hadi kufikia mwaka 2025.

Baada ya idadi ya watalii kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la Uviko-19 mwaka 2020 na 2021, sekta ya utalii sasa inaonekana kurudi kwenye njia ya kufufuka.

Mbali na kupungua kwa vizuizi vya usafiri duniani kote, juhudi za Serikali zimeongeza idadi ya watalii waliofika, kutoka milioni 1.4 mwaka jana.

Mkurugenzi wa utalii katika Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Thereza Mugobi, amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa na serikali ili kuibadilisha sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya utalii.