Rais wa China ajibu barua ya mwenyekiti wa Mfuko wa urithi wa anga kati ya Marekani na China na askari wastaafu wa Flying Tiger
2023-09-20 09:35:06| cri


Rais Xi Jinping wa China amejibu barua ya mwenyekiti wa Mfuko wa urithi wa anga kati ya Marekani na China na askari wastaafu wa Flying Tiger.

Katika barua hiyo, Rais Xi amesema, Mfuko huo unasimulia hadithi za Flying Tiger kwa muda mrefu nchini Marekani, na vijana wengi na watoto nchini Marekani wameshiriki kwenye “Shule ya urafiki ya Flying Tiger” na “Mpango wa viongozi wa vijana”.

Rais Xi amesema maendeleo ya utulivu ya uhusiano kati ya China na Marekani kwenye kipindi kipya yanahitaji kushirikisha na kuungwa mkono na wanachama wa Flyingi Tiger wa kipindi kipya, na kusema anaamini kuwa moyo wa Flying Tiger utaendelea kurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kati ya watu wa nchi hizo mbili.