Wataalamu wa Afrika wasema usalama wa afya ya jamii uko hatarini kutokana na mgogoro wa hali ya hewa
2023-09-20 08:42:48| CRI

Wataalamu wa Afrika wamesema hali tete ya mifumo ya afya barani Afrika imekuwa mbaya zaidi kutokana na majanga ya dharura yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo mafuriko, uhaba wa maji, uchafuzi wa hewa na kuenea kwa haraka kwa virusi vinavyosababisha magonjwa.

Mtaalamu wa kiufundi anayesimamia Ofisi ya Mabadiliko ya Tabianchi na Afya katika Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Brama Kone amesema, kuongezeka kwa joto kumedhoofisha juhudi za bara la Afrika za kukabiliana na mzigo wa magonjwa. Amesema ili kukabiliana na majanga hayo, utekelezaji wa haraka wa matokeo ya Mkutano wa Hali ya Hewa wa Afrika uliofanyika mjini Nairobi, Kenya, ni muhimu katika kuimarisha mifumo ya afya ya bara hilo.

Mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Eldoret nchini Kenya, Melvine Aoko Otieno amesema, nchi za Afrika zinapaswa kuoanisha suala la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na miradi inayoendana nayo kwa lengo la kuboresha afya ya jamii za huko.