Maambukizi ya magonjwa mengi yaenea katika kambi za wakimbizi katika nchi jirani za Sudan
2023-09-20 10:25:33| cri

Tangazo la pamoja lililotolewa na Shirika la Afya Duniani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi limesema tangu mgogoro wa Sudan ulipolipuka, kambi nyingi katika nchi zinazopokea wakimbizi kutoka Sudan zikiwemo Sudan Kusini, Ethiopia na Chad, zimekumbwa na maambukizi ya magonjwa ya aina mbalimbali kama vile kipindupindu, surua, homa ya dengue na malaria, na wakimbizi wengi wanashindwa kupata chakula cha kutosha na maji safi.

Takwimu zimeonyesha kuwa kuanzia tarehe 15 Mei hadi tarehe 14 Septemba, watoto zaidi ya 1,200 wamefariki katika kambi hizo, na kwa sasa kila siku watoto makumi wanakufa kutokana na utapiamlo au surua.