Li Xi afanya ziara rasmi nchini Cuba
2023-09-20 08:39:52| CRI

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Li Xi, amefanya ziara rasmi nchini Cuba na kukutana na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo, akiwemo rais wa nchi hiyo, Miguel Diaz-Canel Bermudezwa.

Rais Bermudezwa ameipongeza China kwa kushirikiana kithabiti na nchi za Kusini, kulinda vizuri maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na kuishukuru China kutoa msaada kwa maendeleo ya uchumi na jamii nchini Cuba. Ameongeza kuwa Cuba inapenda kudumisha mawasiliano karibu na kuhimiza ushirikiano halisi na China

Naye Bw. Li amesema, China inapenda kutekeleza kwa makini makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili, kushughulikia kwa kina mambo ya kichama na kitaifa, na ushirikiano katika sekta mbalimbali, kuendelea kuungana mkono katika maslahi makuu, na kusukuma mbele shughuli za ujenzi wa kichama na kitaifa. Ameongeza kuwa China pia inapenda kushirikiana na Cuba kutekeleza mapendekezo kuhusu maendeleo, usalama na ustaarabu duniani, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.