Watu wanane wauawa katika mapigano makali huko Ogun, Nigeria
2023-09-20 08:32:13| cri

Watu wanane wameuawa katika mapigano makali ya kugombea ardhi katika jimbo la Ogun kusini magharibi mwa Nigeria.

Mkuu wa polisi wa jimbo hilo Bw. Abiodun Alamutu amesema, washukiwa tisa wamekamatwa kufuatia mapigano hayo yaliyotokea katika mji mkuu wa jimbo hilo, Sagamu, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Washukiwa hao tayari wamekiri kuhusika na mapigano hayo makali, na pia washukiwa hao walikutwa na bunduki mbili na risasi kadhaa.