Uchumi wa Rwanda wakua kwa 6.3% katika robo ya pili ya mwaka huu
2023-09-20 09:34:54| cri

Idara ya takwimu ya taifa ya Rwanda (NISR) imesema Rwanda imerekodi ukuaji wa Pato la Taifa kwa 6.3% katika robo ya pili ya mwaka huu kufuatia ukuaji wa 9.2% katika robo ya kwanza.

Taarifa iliyotolewa jana na idara hiyo inaonesha kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa bei za sasa za soko umefikia Faranga bilioni 3,970 ikilinganishwa na Faranga bilioni 3,282 za kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

Ukuaji huo ulichangiwa na sekta ya huduma iliyochangia asilimia 45, kilimo asilimia 27, viwanda asilimia 20, huku kodi ya moja kwa moja ikichangia asilimia 7. Ndani ya sekta ya huduma, biashara ya jumla na rejareja iliongezeka kwa asilimia 6 huku huduma za usafiri zikiongezeka kwa asilimia 8 hasa kutokana na ongezeko la asilimia 23 la usafiri wa anga.

Hata hivyo sekta ya kilimo haikurekodi ukuaji wowote ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.