Mjumbe wa kudumu wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi Balozi Chen Xu, jana alitoa hotuba kwa niaba ya nchi zaidi ya 80 kuhusu masuala ya kulinda haki za wanawake wenye ulemavu kwenye mkutano wa 54 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.
Kwenye hotuba yake Balozi Chen amesema japo sasa mambo yanayohusu wanawake yamepata maendeleo makubwa duniani, lakini wanawake wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uhakikisho wa kijamii, ubaguzi na umaskini.huku ikisisitiza kuwa kuhimiza maendeleo jumuishi ya jamii ni njia muhimu ya kuwanufaisha wanawake hao, ambayo itachangia kuhimiza usawa katika maisha na maendeleo yao.