Rais wa China Xi Jinping amefanya ziara ya ukaguzi mji wa Yiwu mkoani Zhejiang.
Katika ziara yake, alitembelea soko la biashara ya kimataifa la Yiwu ambayo ni “soko kubwa zaidi la biashara ya jumla ya bidhaa ndogo ndogo duniani” na kuhusisha ajira za watu milioni 32. Mwaka jana, thamani ya miamala katika soko hilo ilizidi yuan bilioni 200.
Rais Xi pia ametembelea kijiji cha Lizu cha mji huo ambacho kina familia 333 na kwa jumla watu 706. Miaka ya hivi karibuni, kutokana na kutekelezwa kwa kina kwa mikakati ya “ufufuaji wa vijiji” na kuimarishwa kwa kiwango cha miundombinu, mapato ya wastani ya kila mwanakijiji pale yameongezeka kwa yuan 2,500 kila mwezi, na idadi ya watalii waliotembelea kijiji hicho imefikia zaidi ya laki 2 kila mwaka.