UNHCR yatoa wito wa kuongeza fedha kwa ajili ya wakimbizi wakati mgogoro ukiendelea nchini Sudan
2023-09-21 09:10:22| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema, zaidi ya wakimbizi 400,000 wa Sudan wamewasili nchini Chad tangu mapigano yalipoanza nchini Sudan miezi mitano iliyopita.

Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua, mwakilishi wa Shirika hilo nchini Chad Laura Lo Castro amesema, UNHCR inafanya uratibu pamoja na serikali ya Chad ili kuhakikisha mapokezi, ulinzi na majibu ya mahitaji ya dharura ya kibinadamu kwa wakimbizi hao, na kuongeza kuwa, licha ya juhudi hizo, mahitaji katika kambi ni kubwa na rasilimali zilizopo hazitoshelezi.

Amesema rasilimali zaidi zinahitajika ili kukabiliana na mahitaji ya wakimbizi hao.