China yasema jaribio lolote la kuingilia kati masuala ya Hong Kong halitafanikiwa
2023-09-21 08:35:47| cri


     

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema, China inapinga vikali jaribio lolote la kuingilia kati masuala ya Hong Kong, na kusema kamwe majaribio hayo hayatafanikiwa.

Kauli hiyo imekuja baada ya serikali ya Uingereza ya kutoa ripoti ya nusu mwaka kuhusu suala la Hong Kong. 

Bi. Mao amesema mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, na utekelezaji wa sheria katika Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong unafuata katiba ya China na sheria ya kimsingi ya mkoa huo. Amesema mamlaka ya Hong Kong iliwaadhibu watu walioshukiwa kukiuka Sheria ya Kulinda Usalama wa Taifa ya mkoa huo, na ni hatua inayoendana na haki ya kulinda utawala wa kisheria wa Hong Kong, na pia ni hatua ya lazima ya kulinda usalama wa taifa.