Rais wa Azerbaijan atoa hotuba juu ya hali ya eneo la Nagorno-Karabakh
2023-09-21 14:27:37| cri

Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan ametoa hotuba kuhusu hali ya eneo la Nagorno-Karabakh jana kupitia televisheni.

Rais Aliyev amesema Azerbaijan imetimiza malengo yake yote kwenye operesheni iliyofanywa katika eneo la Nagorno-Karabakh na kurejesha mamlaka yake kwenye eneo hilo, ambapo vikosi vya Waarmenia ambavyo havijaondoka viliangamizwa na vingine vilivyosalia katika eneo hilo vimeanza kujiondoa katika mapigano na kusalimisha silaha. Pia amesema mjumbe aliyemtuma ataeleza “mpango wa kuishi pamoja” kwa wawakilishi wa Waarmenia watakapofanya mkutano.

Upande wa Armenia bado haijajibu hotuba hiyo ya Bw. Aliyev.