Wapiganaji 462 wa al-Shabaab wauawa katika shambulio lililoshindwa
2023-09-21 09:09:35| CRI

Jeshi la Ulinzi la Ethiopia limesema limewaua wapiganaji 462 wa kundi la al-Shabaab katika mji wa Rabdhure, kusini magharibi mwa Ethiopia baada ya wapiganaji hao kujaribu kushambulia kikosi cha Jeshi la Ethiopia lililokuwepo katika eneo hilo.

Katika taarifa yake, Jeshi hilo limesema katika shambulio hilo lililoshindwa, wapiganaji wa al-Shabaab walijaribu kutumia watu 12 wa kujitoa mhanga na magari matatu yaliyotegwa mabomu.

Taarifa hiyo pia imesema, awali Jeshi la Ethiopia lilizuia majaribio kadhaa ya kundi la al-Shabaab kuingia nchini humo na kufanya mashambulio ya kuvuka mpaka.