Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema masuala ya kibinadamu yamekuwa chanzo cha athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi
2023-09-21 09:11:13| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa, ubinadamu ni chanzo cha mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi uliofanyika wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo jana, Guterres amesema joto kali duniani limekuwa na athari mbaya kwa wakulima wanaoshuhudia mazao yao yakisombwa na mafuriko, magonjwa, na maelfu ya watu wakikimbia makazi yao kutokana na mioto ya msituni.

Ameonya kuwa, hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinakabiliwa na changamoto nyingi, na kama hakutakuwa na mabadiliko, dunia inaelekea kukabiliwa na ongezeko la joto la nyuzijoto 2.8, ambalo ni hatari kwa dunia. Ametoa wito wa hatua za kivitendo ili kudhibiti ongezeko la joto duniani kwa nyuzijoto 1.5.