Maonyesho ya Opera ya Wu ya China yafanyika Ethiopia na Kenya
2023-09-21 10:03:33| CRI

 

Ni wakati mwingine tena tunapokutana katika kipindi hiki cha DARAJA kinachokujia kila jumapili kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Kipindi hiki cha Daraja kinakuletea mambo mbalimbali yanayohusiana na China na nchi za Afrika, na ushirikiano wa pande hizo mbili katika sekta mbalimbali, iwe uchumi, biashara, kilimo, ujenzi wa miundombinu na kadhalika. Tutakuwa na ripoti inayohusu maonyesho ya Opera ya Wu ya China ambayo yamefanyika nchini Ethiopia na Kenya, pamoja na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi kuhusu miradi ya kijani kwa Afrika iliyotangazwa na China hivi karibuni katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Afrika.