Rais wa Tanzania awahakikishia usalama wawekezaji wakati akifungua kiwanda cha kioo kilichowekezwa na wachina
2023-09-22 23:03:17| cri

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amewahakikishia wawekezaji usalama wa mali zao na kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji wakati akizindua kiwanda cha kwanza kabisa cha kioo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kioo kilichogharimu dola milioni 311 za Marekani katika wilaya ya Mkuranga, Rais Samia amesema serikali yake itaendelea kuvutia uwekezaji zaidi katika viwanda vikubwa ili kuhimiza sera yake ya kuendeleza viwanda.

Rais Samia amekitaja kiwanda hicho kilichowekezwa na wachina na kuajiri wafanyakazi 750, kuwa ni ushahidi wa ushirikiano mkubwa wa kiuchumi kati ya Tanzania na China, wakati nchi hizo mbili sasa zimehama kutoka kwenye ushirikiano wa kawaida hadi kwenye ushirikiano wa kimkakati.