Chanjo ya majaribio ya Ukimwi kukamilika Juni 2024
2023-09-22 10:04:21| cri

Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr) imesema inatarajia kutoa matokeo ya awamu ya pili ya chanjo ya majaribio ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi mapema mwezi Juni 2024.

Imeelezwa kuwa utafiti wa chanjo hiyo ulianza kufanywa mwaka 2018 katika vituo viwili nchini Tanzania, kikiwepo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr) Mkoa wa Mbeya, na Chuo Kikuu Cha Sayansi Shirikishi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI). Tafiti za chanjo ziko katika awamu tatu ambapo kwa sasa iko katika hatua ya pili ambayo ilianza kufanywa mwaka 2018 na inakamilika Juni 2024.

Serikali ya Tanzania inafanya juhudi kuboresha huduma za afya kwa wananchi, na moja ya hatua hizo ni kuendeleza chanjo dhidi ya magonjwa ya kuambukiza.