Rais Xi Jinping wa China atahudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya 19 ya Asia kesho Jumamosi usiku huko Hangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Zhejiang mashariki mwa China. Katika sherehe hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na CMG na Xinhuanet, Xi atatangaza kufunguliwa kwa Michezo hiyo.