Xi atoa salamu kabla ya sikukuu ya mavuno ya wakulima
2023-09-22 16:32:22| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za dhati kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kwa wakulima na watu wanaofanya kazi katika nyanja za kilimo na wa vijijini kabla ya sikukuu ya sita ya mavuno ya wakulima wa China. Rais Xi amesisitiza kuzingatia lengo la kujenga kilimo imara na kujenga nchi nzuri na yenye utulivu ambayo inafaa kuishi na kufanya kazi.