Rais wa China afanya ziara ya ukaguzi mkoani Zhejiang
2023-09-22 08:37:39| cri


 

Rais Xi Jinping wa China, jumatano wiki hii, amefanya ziara ya ukaguzi kwenye mkoa wa Zhejiang.

Siku hiyo asubuhi, rais Xi alitembelea kijiji cha Lizu na soko la biashara ya kimataifa la Yiwu kwa nyakati tofauti kwenye mji wa Yiwu, Zhejiang, ambapo alifahamishwa hali ya huko kuhusu kuendeleza shughuli zenye umaalumu kutokana na hali halisi ya huko, kuhimiza ustawi wa vijiji na kukuza biashara na nje, na kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu.

Baadaye siku hiyo, rais Xi alikwenda mji wa Shaoxing na kutembelea ukumbi wa maonesho ya “uzoefu wa Fengqiao”, na kufahamishwa maendeleo na uvumbuzi wa “uzoefu wa Fengqiao” kwenye kipindi kipya.

Rais Xi pia alifanya ukaguzi kwenye bustani ya utamaduni wa mfereji wa kale wa Mashariki mwa Zhejiang, na kuelezwa historia ya maendeleo, uhifadhi, na ujenzi wa bustani ya kitaifa ya utamaduni ya mfereji huo.