Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kujenga, kukuza na kudumisha amani kwa wote
2023-09-22 08:38:54| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza katika ujumbe wake wa video kwamba, amani sio tu ni wazo zuri la wanadamu, bali pia wito wa kuchukua hatua.

Guterres amesema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani ambayo huadhimishwa kila Septemba 21. Amesema jamii ya kimataifa inapaswa kujitahidi kujenga, kukuza na kudumisha amani kwa wote. Amesema kwa sasa migogoro imesababisha idadi kubwa ya watu kukimbia makazi yao, na majanga ya moto, mafuriko na joto kali yanaongezeka.

Bw. Guterres pia alisisitiza kuwa, amani haipatikani moja kwa moja, bali ni matokeo ya vitendo, na kutaka kuharakishwa kwa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, na kutumia njia ya diplomasia, mazungumzo na ushirikiano ili kutuliza mivutano na kusitisha migogoro.