China iko tayari kuboresha ushirikiano wa kivitendo na Sierra Leone
2023-09-22 08:39:06| CRI

Makamu wa rais wa China Han Zheng amesema, China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na Sierra Leone katika maeneo mbalimbali na kwa pamoja kuboresha amani ya dunia na maendeleo.

Bw. Han amesema hayo mjini New York, Marekani, alipokutana na rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, kando ya Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Amesema China na Sierra Leone zimekuwa zikiungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya kila upande na masuala mengine muhimu. Kwa upande wake, rais Bio ameishukuru China kwa msaada wake kwa Sierra Leone, na kuongeza kuwa, nchi yake inashikilia kanuni ya China moja, na iko tayari kuongeza ushirikiano wa kivitendo na China katika sekta mbalimbali, na kwa pamoja kulinda uhalali wa maslahi ya nchi zinazoendelea.