Uwekezaji wa China katika nchi za nje waendelea kuongezeka
2023-09-22 08:38:16| CRI

Uwekezaji wa China katika nchi za nje umeendelea kuongezeka katika miezi minane iliyopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.8 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

Msemaji wa Wizara ya Biashara He Yadong amesema, kati ya uwekezaji huo, uwekezaji wa moja kwa moja usio wa kifedha katika nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umefikia dola za kimarekani bilioni 19.2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.5 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo, na thamani ya ujenzi wa miradi iliyofanywa na makampuni ya China katika nchi hizo ilifikia dola za kimarekani bilioni 72.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.8.

He amesema, katika kipindi kijacho, China itajenga vizuri chapa ya “Uwekezaji wa China”, na kuandaa shughuli mbalimbali za “Mwaka wa Uwekezaji wa China”.