Rais Xi Jinping wa China atoa maagizo muhimu juu ya kukuza uchumi mpya wa viwanda
2023-09-23 21:41:59| cri

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alitoa maagizo muhimu kuhusu kukuza uchumi mpya wa viwanda.

Rais Xi alisema katika mchakato wa ujenzi wa nchi yenye nguvu, kukuza viwanda vipya ni kazi muhimu, na inapaswa kuunganisha vizuri ujenzi wa nchi yenye nguvu ya kiviwanda na maendeleo ya uchumi wa kidijitali, ili kuweka msingi imara kwa ajili ya kutimiza mambo ya kisasa kwa njia ya Kichina.