Nchi za Kusini mwa Afrika zakutana Namibia kujadili namna ya kukabiliana na magonjwa ya wanyama ya kuvuka mpaka
2023-09-25 08:44:46| CRI

Mamlaka za mifugo za nchi tano za Kusini mwa Afrika (Namibia, Angola, Botswana, Zambia na Zimbabwe), zimekutana nchini Namibia kujadili namna ya kukabiliana na tishio linaloongezeka la magonjwa ya wanyama ya kuvuka mpaka (TADs) katika eneo hilo.

Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Ofisa Mifugo Mkuu wa Namibia Bibi Albertina Shilongo, amesema mkutano huo kuhusu mambo ya mpaka unaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 27, ni hatua kubwa kuelekea kulinda afya ya wanyama na kukuza ushirikiano wa kikanda.

Bibi Shilongo amesema lengo kuu la mkutano huo ni kupambana na magonjwa ya kuambukiza kama vile pleuropneumonia (CBPP), ugonjwa wa kwato na midomo (FMD), kichaa cha mbwa, na pia wanajadili hali ya wasiwasi kuhusu ongezeko la homa ya mafua ya ndege HPAl.