Kipchoge ashinda Berlin Marathon kwa mara ya tano
2023-09-25 15:02:50| cri

Katika mashindano ya Marathon ya Berlin 2023 yaliyofanyika tarehe 24 mjini Berlin, Ujerumani, mchezaji maarufu wa mbio za masafa marefu wa Kenya Eliud Kipchoge alipata ubingwa kwa kutumia saa 2 dakika 2 na sekunde 41. Hii ni mara yake ya tano kupata ubingwa kwenye Mashindano ya Marathon ya Berlin. Mchezaji wa Ethiopia Tigist Assefa naye amevunja rekodi ya dunia na kujinyakulia ubingwa kwenye mashindano hayo kwa upande wa wanawake kwa kutumia saa 2 dakika 11 na sekende 52.