Kuchimba na kutumia maliasili kwa kujizuia
2023-09-25 15:28:09| CRI

Tunapaswa kupenda mazingira ya asili. "Kuchimba na kutumia maliasili kwa kujizuia" ni kiini cha ustaarabu wa kiikolojia. Tunapaswa kutetea maisha rahisi, ya wastani, yasiyo na uchafuzi na hewa chache ya kaboni, kukataa matumizi kupita kiasi na ufujaji, na kuendeleza maisha ya kistaarabu na mtindo wa maisha unaozingatia afya. Tunapaswa kuongeza ufahamu kuhusu mazingira na ikolojia, kuanzisha mfumo wa kina wa usimamizi wa mazingira unaoshirikisha jamii nzima, na kufanya mwamko kuhusu ulinzi wa mazingira kuwa utamaduni kuu kwenye maisha.