Macron atangaza Ufaransa itaondoa wanajeshi wake nchini Niger ifikapo mwishoni mwa mwaka huu
2023-09-25 23:04:13| cri

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema katika mahojiano ya televisheni kwamba Ufaransa iliombwa na nchi za kikanda kusaidia katika mapambano dhidi ya ugaidi. Kwa vile sasa "utawala halisi nchini Niger" hauko tayari tena kupambana na ugaidi, Ufaransa inaamua kumaliza ushirkiano wa operesheni hii ya kijeshi. Ameongeza kuwa watashauriana na wanajeshi waliofanya mapinduzi (kuhusu kujiondoa) kwa sababu wanataka mambo yaende kwa utulivu.