Msaada wa dharura wa China wasafirishwa kwenda Libya
2023-09-25 09:01:17| CRI

Ndege ya mizigo ya China iliyobeba msaada wa kibinadamu wa dharura wa tani 90 kwa ajili ya Libya, imewasili katika mji wa Benghazi, mashariki mwa nchi hiyo.

Vifaa vya huduma ya kwanza, vifaa vya kusafisha maji, mahema, mablanketi, mifumo ya upimaji wa ultrasound, fulana za uokoaji na vifaa vingine vimesafirishwa hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Benina, na kupokelewa na katibu mkuu wa Shirika la Hilari nyekundu la Libya Bw. Omar Abu-Dabous pamoja na wanadiplomasia waandamizi wa Libya na China.

Septemba 10 dhoruba ya Daniel ilisababisha mafuriko makubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Libya katika miongo kadhaa, na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya eneo hilo, hasa miundombinu ya maji na maji taka.