Ufaransa kuondoa jeshi lake Niger kabla ya mwishoni mwa mwaka huu
2023-09-25 08:43:44| CRI

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametangaza kuwa Ufaransa itaondoa jeshi lake kutoka Niger mwishoni mwa mwaka huu.

Rais Macron amesema Ufaransa inatoa msaada katika mapambano dhidi ya ugaidi kutokana na mahitaji ya nchi za kanda hiyo, sasa mamlaka ya Niger haitaki tena kupambana na ugaidi, kwa hiyo itasimamisha ushirikiano huo wa kijeshi. Ufaransa imesema itajadiliana na maofisa wa jeshi waliofanya mapinduzi nchini Niger kuhusu mambo ya kuondoa jeshi kutoka nchi hiyo, na inataka kazi hiyo ifanyike kwa utulivu.

Rais Macron pia alitangaza kuwa balozi wa Ufaransa nchini Niger atarudi nchini Ufaransa ndani ya saa kadhaa.