Somalia na ATMIS walaani shambulizi la katikati ya Somalia
2023-09-25 08:45:32| CRI

Serikali ya Somalia na Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) wamelaani shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotekelezwa na magaidi wa al-Shabab Jumamosi mjini Beledweyne, katikati mwa Somalia, na kusababisha vifo vya takriban watu 20, na wengine wengi kujeruhiwa.

Katika taarifa tofauti zilizotolewa na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na mwakilishi maalum wa mjumbe wa mwenyekiti Tume ya AU ya Somalia na mkuu wa ATMIS Bw. Mohammed El-Amine Souef, wameahidi kuongeza juhudi za kuleta utulivu nchini Somalia licha ya kuongezeka kwa mashambulizi kutoka kwa kundi la Al- Shabaab.

Rais Mohamud ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu wa watu waliouawa, na salamu za pole kwa majeruhi, na kuahidi kuwa serikali ya Somalia na watu wake hawatakata tamaa katika mapambano yao dhidi ya magaidi na ajenda zao mbaya.