Uwekezaji binafsi wa China wapongezwa kwa kuboresha maisha ya watu nchini Angola
2023-09-25 08:43:59| CRI

Waziri wa nchi za uratibu wa uchumi wa Angola Jose de Lima Massano amepongeza uwekezaji wenye ufanisi uliofanywa na makampuni ya China na athari chanya zitokanazo na kuboresha maisha ya watu nchini humo.

Waziri huyo amesema hayo alipohutubia Mkutano wa Chama cha Biashara kati ya Angola na China (CAC) na makampuni wanachama mjini Luanda. Pia amesisitiza kuwa uwekezaji binafsi wa China si kama tu ni “muhimu kwa nchi hiyo”, bali pia “umetoa nafasi za ajira na kuboresha maisha ya watu kwa kuwapa fursa nzuri za kuongeza mapato.”

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa CAC Luis Cupenala, hivi sasa chama hicho kina makampuni wanachama 112, ambapo mengi kati yao yanatoka sekta binafsi nchini China, na yanafanya kazi katika sekta mbalimbali nchini Angola ikiwa ni pamoja na viwanda, madini, kilimo, uvuvi, na biashara, na yanafanya juhudi kwa maendeleo ya kiuchumi nchini Angola.