Wanasayansi wa China na Kenya wazindua juzuu ya kwanza ya kuhifadhi kumbukumbu mimea ya Kenya
2023-09-26 09:14:07| CRI

Wanasayansi wa China na Kenya wametoa juzuu ya kwanza ya chapisho kuhusu mimea, na kuwa chapisho la kwanza la mimea ya asili la Kenya na kuziba pengo katika eneo la utafiti wa raslimali za mimea nchini Kenya.

Chapisho hilo kuhusu mimea ya Kenya limegawanyika katika juzuu 31, litakuwa na kumbukumbu kuhusu spishi 7000 za mimea kutoka kwa familia 223 za mimea ya Kenya. Huu ni mradi wa ushirikiano kati ya wanasayansi kutoka akademia ya sayansi ya China (CAS), Kituo cha utafiti cha China na Afrika (SAJOREC) na jumba la makumbusho la Kenya.

Mkurugenzi mkuu wa Makavazi ya taifa ya Kenya Bibi Mary Gikungu, amesema kuzinduliwa kwa chapisho hilo ni sehemu ya juhudi za kuhifadhi na kuchochea ukuaji wa kijani nchini Kenya.