Shirika la kibinadamu la Umoja wa Mataifa lalaani mauaji ya madereva wawili wa malori ya utoaji wa misaada nchini Sudan Kusini
2023-09-26 09:11:12| CRI

Wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya madereva wawili wa malori ya utoaji wa misaada na kujeruhiwa kwa mmoja nchini Sudan Kusini mwishoni mwa juma.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema madereva hao walishambuliwa Jumamosi, na malori yao yalichomwa na kuharibiwa wakati walipokuwa wakirejea Juba.

Ofisi hiyo imesema baada ya shambulio hilo, kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesimamisha usafirishaji wa vifaa katika eneo hilo.